Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwezeshaji nchi zinazoendelea ni muarobaini wa mipango inayopitishwa COP21:EAC

Uwezeshaji nchi zinazoendelea ni muarobaini wa mipango inayopitishwa COP21:EAC

Mkutano wa 21 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi ukiendelea huko Paris, Ufaransa, Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC imesema nchi zinazoendelea zinapaswa kuwezeshwa kifedha na kiteknolojia ili mipango inayopitishwa kukabili mabadiliko ya tabianchi iweze kuwa na manufaa na endelevu.

Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa jijini Paris, Ufaransa kando mwa mkutano wa 21 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP21, mtaalamu wa masuala ya kuhimili athari hizo kutoka EAC, Dismas Mwikila amesema..

(Sauti ya Dismas-1)

Bwana Dismass amezungumzia pia wanachotarajia kuhusu fidia kwenye mkataba mpya ikizingatiwa nchi zinazoendelea zinagharimika zaidi kutokana na uchafuzi unaofanywa na nchi tajiri..

(Sauti ya Dismas-2)