Skip to main content

Mradi wa IFAD waboresha familia Zanzibar

Mradi wa IFAD waboresha familia Zanzibar

Nchini Tanzania hususan visiwani Zanzibar, mafunzo ya kuleta usawa wa kijinsia katika familia yameleta manufaa makubwa katika jamii ambapo kwa sasa wake kwa waume wanashirikiana katika kuboresha maisha ya familia. Awali hali haikuwa hivyo kwani majukumu ya kijadi yalipatiwa kipaumbele na kukwamisha maendeleo ya familia. Lakini hali sasa ni tofauti sababu ikiwa ni mradi wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD. Je wamefanya nini? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.