Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP21, mkataba uzingatia haki za binadamu: Mtaalamu

COP21, mkataba uzingatia haki za binadamu: Mtaalamu

Mtaalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na mazingira John Knox, amewakumbusha washiriki wa mkutano wa COP21 huko Paris Ufaransa, kuhakikisha mikakati yoyote ya kukabili mabadiliko ya tabianchi yanazingatia haki za binadamu.

Akizungumza katika mkutano huo leo, Bwana Knox ameyakumbusha mataifa wanachama wa mikataba ya haki za binadamu kuwa, tabianchi ni sehemu ya majukumu ya haki za binadamu ya kila nchi, na kuwataka washiriki kuchukua mtazamo wa haki za binadamu wakati wakijadili masuala ya mazingira.

Amesema hata wanapaswa kuzingatia sheria za haki za binadamu kwa kuwa sasa ni dhahiri kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaathiri vibaya haki za binadamu kiholela na hata kwa wale wasio na mchango mkubwa kwa kusababisha tatizo hilo.

Amesisitiza kuwa ongezeko la haliojoto hata hadi selisiasi mbili kunaathiri vibaya haki za walio hataraini, huko akiwataka washiriki kulenga kudhibiti halijoto katika nyuzijoto 1.5 za selisiasi.