Skip to main content

Siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu yazingatia jamii jumuishi

Siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu yazingatia jamii jumuishi

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya watu wanaoishi na ulemavu, kumefanyika mkutano maalum mjini New York Marekani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza kwamba lengo la ajenda ya maendeleo endelevu ni kuhakikisha kwamba hakuna mmoja anayeachwa nyuma, wakiwemo watu wenye ulemavu. Taarifa kamili na Joseph Msami

(TAARIFA YA MSAMI)

Burudani ya muziki wa ala kutoka kwa washiriki wa Korea katika  iliyoamsha hisia hususani kwa kundi la watu wenye ulemavu  ambalo leo ni siku yao maalum.

Baada ya kuburudishwa Katibu Mkuu Ban  akisisisitiza umuhimu wa kujumuisha watu wenye ulemavu kwenye sera na utekelezaji wao, kuwawezesha na kuwapa haki sawa akisema.  (Sauti ya Ban)

“ Wakati ambapo dunia inajiandaa kutekeleza ajenda ya mwaka 2030, watu wenye ulemavu wanapaswa kutambuliwa kama  walivyo na kwamba  wanaweza kuleta mabadiliko na kuchangia pakubwa kwenye jamii.”

Bwana Ban ameongeza kwamba watu wenye ulemavu usioonekana pia wanapaswa kusikilizwa na kuhudumiwa huku pia viongozi wengine wakitaka dunia kujali masilahi  ya watu wenye ulemavu ikiwamo kuzingatia kundi hilo katika kila sekta ikiwamo huduma za kijamii.