Majanga yakitokea tutoe usaidizi yakinifu: UNFPA Tanzania
Mahitaji ya kiafya ya wanawake na wasichana barubaru mara nyingi hupuuzwa wakati wa harakati za usaidizi wa kibinadamu zinazofanyika baada ya mizozo au majanga.
Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya mwaka huu ya hali ya idadi ya watu duniani iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA iliyopatiwa jina hifadhi baada ya janga.
Mathalani ripoti imesema kati ya watu Milioni 100 wanaohitaji misaada ya kibinadamu duniani kote, Milioni 26 ni wanawake na wasichana walio kwenye umri wa kuweza kupata watoto.
Nchini Tanzania ripoti hiyo imezundiliwa ikiwaleta pamoja wadau wa masuala ya idaidi ya watu na misaada ya kibinadamu hasa ikizingatiwa kuwa taifa hilo limekuwa hifadhi yawakimbizi kutoka nchi kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC na Burundi. Samuel Msoka ni mtaalamu anayesimamia idadi ya watu na maendeleo UNFPA nchini humo
(SAUTI SAMWELI)
Shirika hilo tayari limeanza mipangao ya kusaidia makundi athirika yanapotokea majanga.
(SAUTI SAMUEL)