Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutenga fedha za dharura kabla ya janga kutabadili utoaji wa msaada:WFP

Kutenga fedha za dharura kabla ya janga kutabadili utoaji wa msaada:WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP kwa ushirikiano na mashirika matatu likiwemo lile la msalaba mwekundu la Ujerumani (GRC) yamezindua utaratibu mpya kuhusu utengaji wa fedha kwa ajili ya kujiandaa na kukabiliana na majanga kama njia ya kujenga mifumo ya kukabiliana na majanga

Kwa mujibu wa WFP mpango huo unalenga kubadili huduma ya shirika hilo ya kukabiliana na uhakika wa chakula FoodSECuRE kutoka mfumo wa kukabiliana hadi kuwa mfumo wa kuganga yajayo na kuokoa maisha, fedha na muda.

Kulingana an WFP sio tu kwamba mfumo huu mpya unalinda maisha ya watu bali pia unasaidia kubana matumizi.