Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utekelezaji wa makubaliano ya amani Sudan Kusini ndiyo kipaumbele: Ladsous

Utekelezaji wa makubaliano ya amani Sudan Kusini ndiyo kipaumbele: Ladsous

Baraza la usalama leo limekutana kujadili hali nchini Sudan Kusini ambapo mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani katika Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous amelihutubia baraza hilo akiangazia masuala kadhaa ikiwamo makubaliano ya amani ya taifa hilo.

Amesema usaidizi wa ukomeshwaji wa machafuko ili kufikia utekelezaji wa makubaliano ni kipaumbele na ni lazima ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS usaidie vyama vilivyotia saini makubaliano ya amani ili vifanye kazi pamoja na kuhakikisha usalama hususani mjini Juba .

Bwana Ladsous amesema kutokana na mapendekezo ya jopo la ulinzi wa amani Katibu Mkuu  amependekeza utaratibu wa hatua ambapo amesema mwaka mmoja utatosha kwa UNMISS kutekeleza mabadiliko ya mfumo wa ujumbe huo. Pia ameshauri.

(SAUTI LADSOUS)

‘‘Kuleta amani na utulivu Sudan Kusini kutahitaji juhudi za pamoja kutokwa kwa wadau wote wanaojihusiha na utatuzi wa mgogoro. Baraza la usalama, Muungano wa Afrika, IGAD PLUS na nchi za ukanda huo ambao wana jukumu muhimu katika kutoa msukumo kwa vyama kutekeleza makubaliano na kudhihirisha manufaa ya amani .’’

Kwa upande wake mwakilishi wa kudumu wa Sudan Kusini katika Umoja wa Mataifa Francis Deng amewataka raia wa nchi hiyo kusahau machungu ya vita na kusonga mbele kama taifa.

Amesema nchi hiyo iko tayari kuunda serikali ya umoja wa kitaifa akiwa wadau wataunga mkono majadiliano ya amani