Skip to main content

Msaada wa fedha kutoka Ujerumani kukwamua watoto maeneo yenye vita:UNICEF

Msaada wa fedha kutoka Ujerumani kukwamua watoto maeneo yenye vita:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNICEF linasema mchango wa serikali ya Ujerumani wa kiasi cha Euro milioni 250 mwaka huu, utawafikia mamilioni ya watoto waliotatizika na mizozo.

Taarifa ya UNICEF inasema kuwa fedha hizo zitaelekezwa kwa mweneo ambayo yametahiriwa zaidi na mizozo duniani ikiwamo Afghanistan, Iraq, Libya, Syria, Ukraine na Yemen. Pia fedha hizo zitasaidia watoto wa Syria walioko ukimbizini nchini Jordan, Lebanon na Uturuki.

Mchango huo ni  ongezeko la Euro milioni 150 kutoka kwango cha mwaka jana cha Euro milioni100 kilichotolewa na serikali ya Ujerumani kwa UNICEF.

Msaada huu unakuja wakati huu ambapo takwimu za UNICEF zinasema kuwa zaidi ya watoto milioni 240 wanaishi  katika maeno ya vita duniani, milioni kumi kati yao wakiwa ni kutoka Iraq na Syria.