Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utumwa kikwazo cha haki ya kijamii: ILO

Utumwa kikwazo cha haki ya kijamii: ILO

Utumwa ni uvunjifu wa haki za msingi za binadamu, na kikwazo kikubwa cha haki ya kijamii na hauna nafasi katika karne ya 21 amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kazi duniani ILO, Guy Ryder.

Katika ujumbe wake wa video wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kukomesha utumwa, Bwana Ryder amesema inasikitisha kwamba wanawake na wanaume  milioni 21  wanatumikishwa kazini duniani.

Ameongeza kuwa inasikitisha zaidi kuwa watumikishaji hujipatia fedha haramu zinazokadiriwa kuwa dola bilioni 150 kote duniani huku akitaka utumwa huo pamoja na ule wa majumbani, utumwa wa kingono na kimawazo kukomeshwa.

Bwana Ryder amezisihi serikali kuridhia mkataba wa ILO kuhusu utumikishwaji akisisitiza.

(SAUTI RYDER)

‘‘Ni wakati sasa kwa serikali ambazo kwa wingi zilikubali itifaki hiyo, kutekeleza wajibu wao kwa kuipitisha na kuitekeleza.’’