Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya tabianchi ni mwiba kwa wakulima: FAO

Mabadiliko ya tabianchi ni mwiba kwa wakulima: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema kusaidia sekta ya kilimo katika nchi zinazoendelea ni jambo muhimu ili lengo la dunia la kutokomeza njaa liweze kufanikiwani.

Amesema Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva huko Paris, Ufaransa ambako mkutano wa 21 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP21 unaendelea akisema hatua hiyo ni muhimu kwani familia maskini tayari zinalipa gharama za madhara ambazo wao hawakuchangia.

Martin Frick, Mkurugenzi wa FAO katika idara ya hali ya hewa, nishati na umiliki anaeleza athari za mabadiliko ya tabianchi na mwelekeo wa mvua.

(Sauti ya Frick)

Mabadiliko ya mwelekeo wa mvua yanasababisha wakulima washindwe kulima kwa kuzingatia ufahamu wao wa asili. Kile ulichojifunza kutoka kwa mama au baba yako sasa hakifai tena, au hata hufahamu kuwa kiwango cha joto la usiku kinaweza kuwa nafasi muhimu. Hiyo ndiyo naita janga lisilofahamika kwenye kilimo ambalo linajinasibu kwenye kupungua kwa mavuno na hata kupungua kiwango cha lishe kwenye mazao yako na hilo tayari linatokea sasa.”