Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majadiliano COP21 yanatia moyo: Janos

Majadiliano COP21 yanatia moyo: Janos

Majadiliano kuhusu mkataba wa pamoja wa mabadiliko ya tabianchi katika mkutano kuhusu mada hiyo COP21mjini Paris Ufaransa, yanaendelea ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezindua mkakati wa kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumzia umuhimu wa makabiliano ya madhara ya mabadiliko ya tabia nchi,  Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi Janos Pasztor ameimbia redio ya Umoja wa Mtaifa katika mahojainao maalum mjini Paris Ufaransa kuwa licha ya ya juhudi za sasa lazima ulimwengu utambue kuwa mabadiliko hayo yanaendelea.

Amesema wadau wa mabadiliko ya tabianchi wanatambua umuhimu wa makubaliano yatakayofikiwa katika mkutano wa COP 21 unaeondelea lakini

(SAUTI JANOS)

‘‘Tunahitaji kuwa na uwezo sio tu wa kwendana na mabadiliko, lakini pia kupiga hatua na kuzingatia kuwa hata katika mustakabali hali ya hewa itabadilika. Kwasababu hata ukikomesha hewa chafuzi leo, tayari kuna gesi angani na hali ya hewa itaendelea kubadilika.’’