Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waasi 13 wa ADF wauawa kwenye operesheni ya MONUSCO

Waasi 13 wa ADF wauawa kwenye operesheni ya MONUSCO

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO umeripoti kuwa leo asubuhi umetekeleza operesheni dhidi ya waasi wa ADF karibu na eneo la Eringeti, kwenye jimbo la Kivu Kaskazini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini New York Marekani, msemaji wa umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric amesema operesheni hiyo imefanyika kwa ushirikiano na jeshi la kitaifa la DRC, na kuhusisha helikopta ya mashambulizi na silaha za kivita.

Amesema kwenye operesheni hiyo waasi wapatao 13 wameuawa.