Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yashirikiana na Google kuimarisha upatikanaji wa ramani kwa ajili ya mazingira

FAO yashirikiana na Google kuimarisha upatikanaji wa ramani kwa ajili ya mazingira

Shirika la Chakula na Kilimo duniani, FAO limetangaza kushirikiana na kampuni ya Google Maps  ili kuimarisha upatikanaji wa mbinu za kufuatilia na kuweka kwenye ramani mabadiliko ya tabianchi, matumizi ya ardhi na misitu.

Ushirikiano huo mpya umezinduliwa wakati ambao mkutano wa 21 wa nchi wanachama wa wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP21 ukiendelea mjini Paris Ufaransa.

Kwenye taarifa yake iliyotolewa leo, FAO imesema kwamba teknolojia za kidigitali za kutengeneza ramani zimebadilisha sana jinsi nchi zinapanga matumizi ya rasilimali na kufuatilia uharibifu wa misitu na uenezaji wa majangwa.

Kwa mujibu wa FAO, ushirikano wake na Google Maps utawezesha kukuza ubunifu na utalaam na kusaidia juhudi zote za kutunza mazingira kwa njia endelevu.