Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vizuizi shurutishi dhidi ya Sudan vyaathiri raia kuliko viongozi : mtalaam

Vizuizi shurutishi dhidi ya Sudan vyaathiri raia kuliko viongozi : mtalaam

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na vizuizi vya udhibiti na shurutishi Idriss Jazairy amezisihi leo nchi zinazoweka vikwazo hivyo dhidi ya Sudan kubadilisha sera zao kutokana na hali ya maendeleo iliyoko nchini humo.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo baada ya ziara yake ya siku nane nchini humo, Bwana Jazairy ameeleza kwamba Sudan imekumbwa na vizuizi hivi kwa kipindi cha miaka 20, ambavyo havijaleta mafanikio yeyote.

Licha ya hayo, amesema vizuizi hivyo havijaathiri viongozi, bali raia wa kawaida ambao wameathirika na changamoto kubwa kwenye sekta ya afya, elimu na kiuchumi.

Aidha amekaribisha uamuzi wa kuruhusu uingizaji wa bidhaa muhimu kwa afya, ingawa bado hayajatekelezwa kikamilifu.