Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa kutoa tahadhari mapema, EWS waleta nuru kwa wakazi wa Turkana, Kenya

Mfumo wa kutoa tahadhari mapema, EWS waleta nuru kwa wakazi wa Turkana, Kenya

Katika harakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi jamii ya kimataifa inahaha kujenga uwezo wa jamii kukabiliana na majanga yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ni kwa mantiki hiyo Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP limeanzisha mfumo wa kutoa taarifa za tahadhari kabla ya majanga Climwarn.

Mradi huu ni wa aina yake kwa ajili unalenga jamii zilizoko hatarini. Ungana na Grace Kaneiya katika makala hii inayoangazia utekelezaji wa mradi huo na umuhimu wa kutoa taarifa hizo kwa wakazi wa Turkana nchini Kenya.