Skip to main content

Hoima waadhimisha siku ya Ukimwi kwa huduma bure VVU

Hoima waadhimisha siku ya Ukimwi kwa huduma bure VVU

Mkurugenzi Mtendaji wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na Ukimwi, UNAIDS, Michel Sidibe amepatia mkazo suala la elimu kwa barubaru wa kike na wa kiume kuhusu jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kupima kufahamu iwapo wana virusi vya Ukimwi, VVU au la.

Suala hilo limepatiwa kipaumbele huko Hoima nchini Uganda, hii leo wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambapo huduma hizo zilitolewa sanjari na ushauri nasaha.

Miongoni mwa wanufaika wa huduma hizo ni Julius Agaba.

(Sauti ya Julius)

Nchini Tanzania, Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS Warren Naamara amemweleza Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa kile wanachofanya kupitia siku ya Ukimwi.

(Sauti ya Naamara)