Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 70,000 huambukizwa VVU nchini Tanzania kila mwaka:UNAIDS

Watu 70,000 huambukizwa VVU nchini Tanzania kila mwaka:UNAIDS

Mkurugenzi mkazi wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na Ukimwi, UNAIDS nchini Tanzania, Warren Naamara amesema maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ni fursa nzuri ya kukumbusha watu kuwa ugonjwa huo upo na hivyo ni vyema kuchukua hatua stahiki mapema iwezekanavyo.

Akihojiwa na Stella Vuzo wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo, Bwana Naamara amesema hatua hiyo ni muhimu kwa kuzingatia takwimu za vifo na maambukizi nchini Tanzania.

(Sauti ya Naamara)

Alipoulizwa kuhusu nchi inayoongoza Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi barani Afrika, Mkurugenzi mkazi huyo wa UNAIDS nchini Tanzania amesema..

(Sauti ya Naamara)