Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP21: juhudi za viongozi wa Afrika zamulikwa

COP21: juhudi za viongozi wa Afrika zamulikwa

Mkutano wa 21 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP21 ukiendelea mjini Paris Ufaransa, viongozi wa Afrika wamekutana kwenye mkutano maalum ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewaambia kwamba bara la Afrika ndilo linalotegemea zaidi tabianchi katika uchumi wake, hasa kilimo.  Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Katika hotuba yake, Ban amesema Afrika imeshapiga hatua kubwa katika kupunguza umaskini kwa njia rafiki kwa mazingira, na kulipa kipaumbele suala la mabadiliko ya tabianchi.

Amesisitizia sekta ya nishati akionyesha jinsi nchi nyingi za Afrika zimechukua fursa ya nishati mbadala na endelevu kwa ajili ya kutimiza mahitaji ya wananchi wake..

Hatimaye ametoa wito kwa viongozi :

(Sauti ya Ban )

"Bado maswala ya msingi ya kisiasa hayajatatulliwa. Kuna kazi nyingi hapa Paris, na changamoto ni kubwa hasa kwa watu na nchi zilizo kwenye mazingira magumu zaidi. Wanasayansi wametuambia kwamba tumebakisha miaka michache kabla kushindwa kuzuia athari kubwa na hatarishi zaidi za tabianchi."