Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuongeze kasi ili tutokomeze Ukimwi, uwezo tunao: Ban

Tuongeze kasi ili tutokomeze Ukimwi, uwezo tunao: Ban

Maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani mwaka huu yanakuja kukiwa na matumaini mapya na pongezi zangu nyingi kwa wanaharakati. Ndivyo alivyoanza Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye ujumbe wake wa siku ya ukimwi duniani hii leo. Taarifa zaidi na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Amesema harakati hizo zimesababisha mafanikio katika kukabili ugonjwa huo duniani ikiwemo utashi wa kisiasa miongoni mwa viongozi, wanasayansi na hata kuwapatia matumaini wale wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Hata hivyo amesema hatua zinahitajika zaidi ili kuongeza idadi ya watu wanaopata matibabu ay kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi ili ifikie Milioni 37.

Halikadhalika huduma za kinga kwa vijana barubaru wa kike na wa kiume sambamba na wajawazito ili waweze kujifungua watoto wasio na virusi vya Ukimwi.

Ban amesema ni matumaini yake kuwa mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi hapo mwakani utakuwa ni fursa kwa viongozi wa dunia kuazimia kasi mpya ya kutokomeza Ukimwi.