Uwekezaji zaidi wahitahijika kutokomeza Ukimwi: Simin

Uwekezaji zaidi wahitahijika kutokomeza Ukimwi: Simin

Ikiwa leo Disemba Mosi, dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya Ukimwi  msisitizo ukiwa zaidi katika upatikanaji wa matibabu yanayopunguza makali ya virusi vya ugonjwa huo (ARV), imeelezwa kuwa uwekezaji katika kuukabili ugonjwa huo bado unahitajika.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York, Marekani, mkurugenzi wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na Ukimwi, UNAIDS, ofisi ya New York, Simin Bland amesema licha ya mafanikio kwa ujumla ya kukabiliana na Ukimwi kupitia malengo ya maendeleo milenia, MDGs, bado kuna mengi ya kufanya.

Amesema ili kufikia malengo sambamba na ajenda 2030 ya maendeleo endelevu SDGS, uwekezaji wa kifedha zaidi unahitajika.

(SAUTI SIMIN)

‘‘Ikiwa tunataka  kuwanyemuelekeo  kufikia malengo ya 2030 , tunahitaji kuwekeza zaidi ya tunavyofanya leo, tunakadiria kimataifa tunahitaji uwlezaji wa kiasi cha doal bilioni 20 hadi 22. Tunakadiria kuwa hadi mwaka 2020 tumahitajikiasi cha kati aya  dola bilioni 30 na 31.’’

Amesema kila mwaka kuna wagonjwa wapya Milioni mbili kote duniani wanaoambukizwa HIV jambo linalohitaji hatua zaidi kuchukuliwa.