Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafanikio ya COP21 ni jukumu la viongozi: Ban Ki-moon

Mafanikio ya COP21 ni jukumu la viongozi: Ban Ki-moon

Leo ikiwa ni siku ya kwanza ya Kongamano la Kimataifa la Tabianchi COP21 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekutana na marais wa nchi mbali mbali duniani wanaoshiriki mkutano wa viongozi, akikariri wito wake kwa viongozi hao kwamba wanawajibika ili kufanikisha makubaliano juu ya mabadiliko ya tabianchi.

Amesema ujumbe wa COP21 ni kwamba mabadiliko ya uchumi wa kimataifa kuelekea uchumi rafiki kwa mazingira yameshaanza na yatanufaisha watu wote.

Aidha Bwana Ban amesisitiza kwamba viongozi wa dunia wanapaswa kuyapa kipaumbele manufaa ya umma, akiongeza kwamba kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi ni manufaa ya kila nchi na amewasihi viongozi hao waafikiane bila kuacha jukumu hilo kwa viongozi wa kizazi kijacho.

Kwa upande wake Rais Barack Obama wa Marekani,nchi ya pili duniani kwa kutoa gesi chafuzi ametaja madhara yanayoweza kutokea iwapo hatua hazichukuliwi kama vile mafuriko yanayosababisha watu kusaka hifadhi kwenye nchi nyingine na kwamba..

(Sauti ya Obama)

Mustakhbali wa aina hiyo siyo tu kwa nchi thabiti wala kwa nchi maskini ambazo zinaweza kustahimili!  Mustakhbali huo ni ule ambao  tuna uwezo wa kubadili hapa hapa na wakati huu, lakini ni iwapo tutakabili changamoto hizi.”