Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Ufaransa

Ban akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Ufaransa

Kuelekea mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi hapo kesho mjini ParisCOP21,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Ufaransa François Hollande, ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo.

Bwana Ban amemshukuru kiongozi huyo kwa ujasiri wake wa  kuandaa mkutano huo licha ya mashambulio ya kigaidi nchini Ufaransa hivi karibuni pamoja na kumshukuru kwa uongozi wake katika suala la mabadiliko ya tabia nchi.

Viongozi hao wawili pia wamejadili kwa kina makubaliano kuhusu kupitishwa kwa mkataba wa Paris na kubaini kuwa masuala nyeti bado yanajadiliwa. Wamekubalina kuwa kushindwa kufikia makubaliano sio matarajio na hilo laweza kusababisha madhara.

Ban na Rais Hollande wa Ufaransa wamejadili pia suala la mapambano dhidi ya  ugaidi ambapo Katibu Mkuu amemweleza Rais huyo kuwa atawasilisha mpango mkakati wa kukabiliana na ugaidi na vikundi vyenye misismamo mikali na kueleza matumaini yake kuwa Ufaransa itaunga mkono azimio hilo.