Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ana matumaini na COP21

Ban ana matumaini na COP21

Siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi huko Paris, UFaransa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema ana matumaini kuwa viongozi wa dunia watapitisha makubaliano stahili kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa, jijini Paris, Bwana Ban amesema matumaini hayo yanazingatia kuwa wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii na wakati wa hatua ni sasa kwani madhara yake yako dhahiri...

(Sauti ya Ban)

“Tumeshuhudia madhara makubwa ambayo yameathiri dunia nzima, iwe nchi maskini au tajiri! Madhara hayajali mipaka,  hili ni suala la dunia. Kwa hiyo sasa wanatambua kuwa kuwekeza vyema katika miradi ya kudhibiti mabadiliko ya tabianchi kutasaidia kuinua uchumi. Nchi nyingi sasa zinawekeza katika nishati endelevu ikiwemo nishati ya jua na hili ni  jambo linashamiri sana, na viongozi wa sekta ya kibiashara imekuwa makini sasa kuwa biashara zao zitakuwa katika mwelekeo bora zaidi iwapo watazingatia mabadiliko ya tabianchi.”

Zaidi ya viongozi 150 watashiriki mkutano huo huku nchi 180 zikiwa zimewasilisha michango yao ya kitaifa ya kudhibiti mabadiliko ya tabianchi.