Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunaweza kutokomeza Polio:Ban

Tunaweza kutokomeza Polio:Ban

Akiwa nchini Malta Katibu Mkuu wa Umoajwa Mataifa Ban Ki-moon amezungumzia umuhimu wa kupambana na ugonjwa wa Polio unaosababisha  kupooza kwa viungo vya mwili akisema ushirikiano wa sekta mbalimbali unahitajika katika kutokomeza ugonjwa huo.

Ban amesema jamii nzima  inahitaji kushiriki vita hiyo  wakiwamo viongozi wa serikali, viongozi wa dini na wale wa kimila, vijana na makundi mengine.

Amesema wanawake pamoja na makundi vya kijamii kama vile wasomi, wafanyabiashara na wengineo pia wanahitajika kushirikia ili kuitokomeza Polio huku akishauri pia kuwa katika sehemu ambazo kuna mizozo lazima pande kinzani kuruhusu wafanyakazi wa afya ili waweze kutoa chanjo ya Polio kwa watoto.

Akitolea mfano,  Ban amesema Nigeria imeonyesha mfano mzuri kufuatia kutangazwa na shirika la afya ulimwenguni WHO, kuwa  haina Polio. Ametaka jumuiya ya kimataifa kuchangia fedha za kuwezesha makabiliano  dhidi ya ugonjwa huo na kutimiza ahadi kwa watoto duniani