Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Askari wawili walinda amani wauwawa Mali , Ban alaani

Askari wawili walinda amani wauwawa Mali , Ban alaani

Askari wawili walinda amani na raia ammoja ambaye ni mhandisi wameuwawa nchini Mali kufuatia shambulio katika kambi ya Umoja wa Mataifahuko Kidal Jumamosi.

Katibu Mkuu Ban Ki-moon amelaani tukio hilo ambalo kwa mujibu wa ujumbe wa UM nchini humo MINUSMA limejeruhi watu 20, wanne kati yao vibaya.

Katika taarif a yake Ban ametuma salamu za rambirambi kwa watu na serikali ya Guinea na Bukinafaso wanakotoka marehemu na kusema kuwa shambulio hilo haitarudisha nyuma juhudi za Umoja katika kufikia makubaliano ya amani.

Kwa mujiu wa MINUSMA hakuna kikundi kilichodai kuhusika na shambulio hilo ambapo Ban amesisitiza umuhimu wa kuwafikisha mahakamani watekelezaji wa tukio hilo.