Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

#WRC15 yafikia ukomo, Afrika yatetea msimamo wake:

#WRC15 yafikia ukomo, Afrika yatetea msimamo wake:

Hatimaye pazia la mkutano wa masafa ya radio limefungwa huko Geneva, Uswisi baada ya takribani mwezi mmoja wa majadiliano kuhusu masafa hayo kwa maslahi ya wakazi wa dunia hii. Mambo kadha wa kadha yamejadiliwa na kuridhiwa na nchi 160 kati ya 193 wanachama wa shirika la mawasiliano duniani, ITU mwenyeji wa mkutano huo. Je ni yapi hasa yalijadiliwa? Nchi za Afrika zimeondoka vipi kwenye mkutano huo? Kufahamu hayo na mengine mengi, Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza kwa njia ya simu na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania, TCRA Dkt. Ali Yahya Simba ambapo hapa anaanza kwa muhtasari wa yale muhimu yaliyojiri.