Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo vya barubaru vitokanavyo na Ukimwi vyaongezeka: UNICEF

Vifo vya barubaru vitokanavyo na Ukimwi vyaongezeka: UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema kwamba idadi ya vifo vya vijana barubaru itokanayo na maambukizi ya virusi vyaUkimwi imeongezeka mara tatu katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.

Ukimwi unaongoza kwa kuuwa barubaru  wengi barani Afrika na ugonjwa huo ni wa pili kwa kusababisha vifo vya kundi hio duniani. UNICEF imesema kati ya idadi ya watu waliomabukizwa Ukimwi, kiwango cha maambukizi hakipungui kwa kundi hili ikilinganishwa na makundi mengine.

Katika mkutano mjini Afria Afrika Kusini hii leo mkuu wa HIV/AIDS katika UNICEF Craig McClure, amesema ni muhimu vijana  barubaru wenye maambukizi wapate matibabu na usaidizi.

Kwa mujibu wa takwimu hizo ukanda wa Kusini mwa jangwa la Sahara unaongoza kwa maambukizi ambapo wasichana saba kati ya kumi wamepata maambukizi mapya hii ikiwa ni kati ya umri wa miaka 15 hadi 19.