Ukatili Sudan Kusini wagharimu zaidi maisha ya watoto:Beah

27 Novemba 2015

Mwendelezo wa ghasia na vitendo vya ukatili vinavyoendelea huko Sudan Kusini vimezidi kuwa na madhara makubwa kwa maisha ya watoto nchini humo.

Hiyo ni kauli ya mtetezi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa watoto walioathiriwa na vita Ishmael Beah watoto walioathiriwa na vita, Ishmael Beah aliyotoa baada ya kuhitimisha ziara ya wiki moja nchini humo.

Akiwa nchini humo alipata fursa ya kukutana na watoto waliokuwa wametumikishwa vitani ambapo amesema kiwango cha ukatili na idadi ya watoto waliohusika moja kwa moja kwenye mapigano nchini humo imeongezeka mwaka huu.

Akizungumzia hali hiyo, mwakilishi wa UNICEF nchini Sudan Kusini Jonathan Veitch amesema kinachoendelea sasa siyo matarajio ya wananchi miaka minne iliyopita wakati wakifurahia uhuru.

Amesema miaka miwili ya mzozo ni dhahiri kuwa imegharimu mambo mengi ikiwemo maisha ya watu na fursa za maendeleo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter