Vikundi vilivyojihami vyatumia mabomu ya ardhini:Ripoti

26 Novemba 2015
Ripoti mpya kuhusu ufuatiliaji wa matumizi ya mabomu ya kutegwa ardhini imeonyesha ongezeko la matumizi ya mabomu hayo hususan na vikundi haramu vilivyojihami.
Ikiwa imeandaliwa na taasisi ya kimataifa inayofanya kampeni dhidi ya mabomu ya ardhini, ICBL, ripoti hiyo yam waka huu imetolewa leo Geneva, Uswisi na kutaja pia ongezeko la idadi ya majeruhi ikilinganishwa na miaka tisa iliyopita.
Jeff Abramson, Meneja wa ufuatiliaji ambaye pia ni Mhariri mkuu wa ripoti hiyo amesema, matumizi mapya na majeruhi kutokana na mabomu hayo yamerudisha nyuma hatua zilizopigwa na dunia katika miaka iliyopita.
Ameongezea kuwa juhudi zaidi zinatakiwa kuharibu mabomu ya kutegwa ardhini katika maeneo husika ili kuzuia vikundi vilivyojihami kuyatumia.
Mabomu hayo yalitumiwa zaidi katika nchi zenye migogoro zikiwemo Afghanistan, Ukraine, Iraq na Yemen kati ya Oktoba 2014 na Oktoba 2015, imesema ripoti hiyo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter