Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndoa za utotoni Afrika kuongezeka maradufu hadi Milioni 310 ifikapo 2050: UNICEF

Ndoa za utotoni Afrika kuongezeka maradufu hadi Milioni 310 ifikapo 2050: UNICEF

Hali ya sasa ikiendelea bila hatua kuchukuliwa, idadi ya watoto wa kike wanaoolewa katika umri mdogo barani Afrika itaongezeka maradufu na kufikia Milioni 310 ifikapo mwaka 2050.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya takwimu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iliyotolewa leo ikisema sababu ni kasi ndogo ya kudhibiti ndoa hizo na kasi kubwa ya ongezeko la idadi ya watu.

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Anthony Lake amesema idadi hiyo ikiangaziwa na athari zake ni kwamba mtoto huyo anakuwa amepoteza maisha ya utoto halikadhalika mustakhbali wake na kama hivyo haitoshi watoto wanaozaliwa an watoto wenzao wanakumbwa na matatizo makubwa ya afya ikiwemo kuzaliwa njiti.

Kwa hivyo ni amesema ni vyema hatua zichukuliwe ili ndoa za utotoni zitokomezwe mara moja hasa nchi maskini ambako uwezekano wa mtoto wa kike kuolewa bado ni mkubwa zaidi kama ilivyokuwa miaka 25 iliyopita.