Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kinachoendelea Ethiopia ni janga : Kang

Kinachoendelea Ethiopia ni janga : Kang

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mratibu wa ofisi ya Umoja huo ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, Bi  Kyung-wha Kang amesema hali ya ukame inaikumba  Ethiopia,  hatua inayohitaji msaada wa kibinadmau wa haraka.

Bi Kang ambaye ametembelea nchi hiyo hivi karibuni na kujionea mahitaji ya kibinadamu, amekutana na waandishi wa habari mjini New York  na kusema  kuwa ukame nchini Ethiopia ni  matokeo ya  athari za El nino na kwamba takribani watu milioni nane wanahitaji msaada wa chakula.

Amesema licha ya jitihada za serikali  lakini mengi yanahitajika kufanyika.

(SAUTI KANG)

‘‘Wanajamii waanatambua msaada unatolewa na serikali katika ugawaji wa chakula, lakini wanahitaji zaidi na wanachohitaji sio chakula cha kuwanusuru leo,  lakini suluhisho la kudumu.’’

Kwa mujibu wa Bi Kang,  kiasi cha dola milioni 200 kimetumika ikiwa ni mchango wa wafadhili lakini akasisitiza kuwa kiasi cha dola bilioni moja zinahitajila ili kunusru maisha ya raia.