Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Papa Francis kuzuru makao makuu ya UM nchini Kenya

Papa Francis kuzuru makao makuu ya UM nchini Kenya

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis ambaye yuko ziarani nchini Kenya, baadaye leo atatembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye viunga vya mji mkuu Nairobi Alhamisi.

Kwa mujibu wa ratiba, Papa Francis ambaye anazuru bara la Afrika kwa mara ya kwanza atakaribishwa katika makao makuu ya Umoja huo huko Gigiri na Mkurugenzi Mkuu Sahle-Work Zewde.

Akiwa kwenye eneo hilo atapanda mti karibu na jengo la Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP akiwa ameandamana na mkuu wa shirika hilo Achim Steiner na hatimaye kuhutubia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wanadiplomasia.

Ziara hiyo Kenya ni sehemu ya ziara yake ya nchi tatu barani Afrika. Nchi zingine atakazotembelea ni Uganda na Jamhuri ya Afrika ya kati.