Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili dhidi ya wanawake haukubaliki: Ban

Ukatili dhidi ya wanawake haukubaliki: Ban

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake, wadau wa harakati dhidi ya haki za wanawake wamekutana na katika tukio maalum hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa  la kuadhimisha siku hiyo. Assumpta Massoi na maelezo kamili.

(TAARIFA YA  ASSUMPTA)

Nats..

Video maalum inayoonyesha juhudi za kukabiliana na ukatili dhidi ya wanwake ikionyeshwa katika ukumbi huu ulioshamiri rangi ya chungwa kwa mavazi ya washiriki ambayo ni mahususi kwa ajili kuangazia utokomezwaji wa ukatili dhidi ya wanawake.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye amejinasibu kama kiongiozi anayetoa kipaumbele  kwa wanawake katika uongozi kwake ikiwa ni pamoja na kuwezesha  kampeni ya kuwajumuisha wanaume katika ukombozi dhidi ya ukatili kwa wanawake,  ijulikanayo kama He for she, amesema wanawake ni mawakala wa mabadilko na hivyo ukatili dhidi yao ukomeshwe ili kutoa fursa kwa kundi hilo kushiriki katika ustawi wa jamaii katika nyanja zote huku akitaja baadhi ya masahibu wanayokumbana nayo.

(SAUTI BAN)

’Tumeona mashambulizi katili mathalani dhidi ya mtoto Malala na wanafunzi wenzake, kutekwa kwa watoto wa Chibok Nigeria, hofu wanayopata wanawake  hususani makundi madogo huko Syria, Iraq na sehemu nyinginezo.’’

Kwa upande wake Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la wanawake, UN Women Phumzile Mlambo Ngcuka anasema wanawake wanaweza kuwezeshwa kwa njia nyingi mathalani.

(SAUTI PHUMZILE)

‘’Kupitia vikundi vya kijamii, vinavyotoa elimu kwa wanaume kuhusu uwiano usio sawa unaokuza  ukatili dhidi ya wanawake, kupitia vikundi vya kiutamaduni na michezo katika ngazi mbalimbali. ‘’

Siku 16 za harakati dhidi ya ukatili kwa wanawake imeanza leo kote duniani.