Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuangalie upya matumizi ya viua wadudu: FAO

Tuangalie upya matumizi ya viua wadudu: FAO

Leo ikiwa ni miaka thelathini tangu kuzinduliwa kwa Muongozi wa Kimataifa wa Shirika la Kilimo na Chakula duniani, (FAO) kuhusu matumizi ya madawa ya kuulia wadudu, shirika hilo limetoa wito kwa mataifa kuhakikisha kuwa mifumo ya kudhibiti na kusimamia matumizi ya madawa hayo inazingatiwa John Kibego na taarifa zaidi.

(Taarifa Kibego)

Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa FAO kuhusu kilimo na usalama wa mtumiaji Ren Wang amesema, licha ya kuwepo mafanyikio tangu kupitishwa kwa muongozi na kanuni hizo, bado mifumo mingi ya kitaifa kuhusu usimamizi wa viua wadudu inahitaji kurekebishwa ili kudhibiti changamoto zilizopo sasa.

Amesema kwa sasa mambo mengi yanafahamika kuhusu madhara ya muda mrefu ya viua wadudu kwa afya na mazingira na kwamba usimamizi mbaya wa viua wadudu unaweza kuathiri vibaya biashara ya mazao ya kilimo.

Wang ameonya kuwa, sheria ya kudhibiti viua wadudu ya miaka ya 80 inahitaji kupitiwa kwa sababu za afya ili kuhakikisha kwamba nchi zinalinda watu na mazingira yake.

Amesema, soko la kimataifa la viua wadudu limenoga maradufu katika kipindi cha miaka 15 iliyopita na kwa sasa mauzo yake ya kila mwaka ni dola bilioni hamsini