Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madawati ya jinsia na ukombozi dhidi ya ukatili kwa wanawake Tanzania

Madawati ya jinsia na ukombozi dhidi ya ukatili kwa wanawake Tanzania

Harakati za kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto huko Tanzania nako zinashika kasi ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UN-Women linashirikiana na jeshi la polisi kuanzisha madawati ya jinsia na watoto kwenye vituo vya polisi.

Hadi sasa kuna madawati hayo 417 katika vituo vyote vya polisi nchini Tanzania ambapo mkuu wa dawati la jinsia na watoto makao makuu ya jeshi la polisi nchini humo Pili Nyamandito anasema yamekuwa na manufaa.

(Sauti ya Pili)

Maelezo zaidi kuhusu madawati ya jinsia nchini Tanzania utapata kwenye jarida letu maalum kesho Alhamisi.