Skip to main content

Mabadiliko ya tabianchi yaathiri mamilioni ya watoto: UNICEF

Mabadiliko ya tabianchi yaathiri mamilioni ya watoto: UNICEF

Ripoti iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF mbele ya mkutano wa 21 kuhusu mabadiliko ya tabianchi ujulikanao kama COP21 mjini Paris, Ufaransa, inasema, zaidi ya watoto nusu bilioni duniani kote huishi katika maeneo yenye mafuriko makubwa, huku milioni 160 wakiishi kwenye maeneo ya  ukame kali.

Milioni 300 kati ya milioni 530 wanaishi katika mataifa ambako nusu ya wanchi wanakabiliwa na umaskini uliokithiri.

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Anthony Lake amesema hatua za dharura zahitajika kuitikia hali hii, akiongezea kuwa watoto wanachangii kidogo  zaidi kwa mabadiliko ya tanbianchi ilihali wao na watoto wao wataishi kukabiliwa na athari mbaya zake.

Bwana Lake amesema, ni wajibu wa wahudhuriaji wa mkutano wa COP21 kufanya maamuzi sahihi kingia watoto na sayari, kwani tayari wanafahamu chakufanya kuzuia majanga yatokanayo ya mabadiliko ya tabianchi.