Skip to main content

Ban alaani shambulio nchini Tunisia

Ban alaani shambulio nchini Tunisia

Katibu Mkuu wa Umoaj wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio lililotekelezwa leo nchini Tunisia dhidi ya basi lilolebeba walinzi wa Rais na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu inasema kuwa Bwana Ban ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waathiriwa, watu na serikali ya Tunisia.

Amesisitiza kuwa Umoaj wa Mataifa utaendelea  kusaidia Tunisia katika mapambanao dhidi ya ugaidi na kukuza demokrasia