Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bangladesh:Ofisi ya haki za binadamu yalaani kunyongwa kwa watuhumiwa

Bangladesh:Ofisi ya haki za binadamu yalaani kunyongwa kwa watuhumiwa

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu imelaani mauaji ya Salauddin Quader Chowdury na Ali Ahsan Mohammad ambao wamenyongwa jumapili hii nchini Bangladesh baada ya kuhukumiwa kifo kwenye kesi ya mauaji ya kimbari na mauaji dhidi ya kibinadamu yaliyofanyiwa mwaka 1971.

Taarifa ya ofisi hiyo iliyotolewa leo imesema kwamba watu 15 kutoka Chama cha Kitaifa cha Bangladesh na Jamaat-e-Islamu wamehukumiwa adhabu za kifo na Mahakama ya Mauaji ya Kimataifa ya Bangladesh tangu kuanzishwa kwa mahakama hiyo mwaka 2010.Ofisi ya Haki za Binadamu imependekeza kwamba adhabu hizo zisitekelezwe kwa sababu ya mashaka kuhusu usawa ya kesi hiyo.

Hali kadhalika Ofisi hii imekariri kwamba inapinga matumizi ya adhabu ya kifo kwenye kesi zozote, hata kwa mauaji mabaya sana.