Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa kilimo wapambana na mabadiliko ya tabianchi Rwanda

Mradi wa kilimo wapambana na mabadiliko ya tabianchi Rwanda

Nchini Rwanda, hali ya hewa haitabiriki kama zamani; sababu ni mabadiliko ya tabianchi ambayo yameathiri mfumo wa mvua nchini humo huku wanasayansi wakikadiria kwamba wakulima wako hatarini kupoteza hadi asilimia 90 ya mavuno yao kutokana na shida hiyo. Ili kukabiliana na hali hiyo, mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD pamoja na serikali ya Rwanda umeanzisha mradi wa kuwezesha wakulima nchini humo na kuwasaidia kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Tayari mafanikio yamepatikana kama anavyosimulia Priscilla Lecomte kwenye makala hii.