Ili kukabiliana na umaskini ni lazima LDCs ziweke malengo mahsusi:UNCTAD

24 Novemba 2015

Katika kongamano la nne la Umoja wa Mataifa la nchi zinazoendelea lililofanyika Istanbul, Uturuki mwaka 2011, wakuu wa mataifa walikubaliana kuwa hatua zimepigwa katika nchi zinazoendelea LDCs katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Hata hivyo, walielezea wasiwasi wao kuhusu umaskini wa kiwango cha juu na njaa katika nchi hizo na hivyo wakaahidi kusaidia zile zenye  uchumi wa chini kuweza kupiga hatua.

Biashara inatajwa kama moja ya muarobaini wa kukabiliana na changamoto ambazo mataifa yanayoendelea yanakumbana nayo. Lakini uwezo wa biashara kumaliza umaskini unasalia ndoto tu. Hayo ni baadhi ya mambo  yaliyomo katika ripoti ya kila mwaka ya kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD kuhusu LDCs na kufahamu kwa kina zaidi Grace Kaneiya wa Idhaa hii amezungumza na Mukhisa Kituyi ambaye ni Katibu Mkuu wa UNCTAD na anaanza kwa kuelezea mambo muhimu katika ripoti hiyo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud