Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vichochezi kwa wapiganaji mamluki vyaangaziwa

Vichochezi kwa wapiganaji mamluki vyaangaziwa

Kamati dhidi ya ugaidi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imekuwa na mkutano hii leo kati yake na watafiti kuchambua na kujadili masuala ya  ugaidi ikiwemo wapiganaji wa kigeni au mamluki.

Akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa kamati hiyo Balozi Raimonda Murmokaite amesema ugaidi hauna nafasi yoyote ile duniani na hakuna jambo lolote linaloweza kutumika kuhalalisha huku akigusia suala la wapiganaji mamluki..

(Sauti ya Balozi Raimonda)

“Jambo hili la wapiganaji mamluki limeendelea kuwa ni mwiba na la wasiwasi mkubwa kwa nchi wanakota, kule wanakopita na hata kule wanakofikia na vile vile maeneo ya mipakani ambako kuna mizozo. Katika maeneo hatarishi zaidi duniani wapiganaji hawa wamekuwa vichochezi vya ukosefu wa usalama na kueneza ukosefu wa usalama wa kisiasa.”

Mmoja wa watoa mada Profesa Scott Atran ameangazia kile kinachochochea watu kujiunga na vikundi vya kigaidi ikiwemo watoto ambapo amesema..

(Sauti ya Atran)

 Idadi kubwa ya wapiganaji wa kigeni wanaojiunga na ISIL wanfanya hivyo kwa hiari, hasa wanaotoka Ulaya na nje Mashariki ya Kati. Wale wadogo wanaojiunga kwa ujumla hawana ufahamu sana wa dini. Wengi wanaojiunga wako katika kipindi cha mpito cha maisha yao, pengine ni wanafunzi au wanasaka kazi, katika umri wa labda miaka 18 au 20 na  wanakuwa wamekimbiai familia zao za awali na kusaka familia mpya miongoni mwa marafiki au wasafiri wenzao ambako wanaona  wanaweza kujiona wanatambuliwa.”