Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajira ni suluhu dhidi ya misimamo mikali: UNDP

Ajira ni suluhu dhidi ya misimamo mikali: UNDP

Mbinu mpya ya kupambana na itikadi ya misimamo mikali inayozaa ugaidi ni kuziba mianya ya ukosefu wa ajira na kubadili itikadi za wahusika, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP.

Katika mkutano wa siku moja mjini New York ulioandaliwa na UNDP na kujadili namna ya kupambana na misimamo mikali na ugaidi katika muktadha wa ajira, Mratibu wa Afrika wa programu hiyo Mohamed Yahya ameiambia idhaa hii kuwa upatikanaji wa ajira ni muhimu kwani mbinu ya makabiliano ya silaha pekee dhidi ya itikadi haiwezi kuzaa matunda kwa hiyo.

(SAUTI MOHAMED)

Amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la vijana kujiunga na vikundi vyenye misimamo mikali na hivyo kuna haja ya kushirikisha wadau wengi zaidi.

(SAUTI MOHAMED)