Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa nchi za kipato cha chini umeendelea kupungua:Ripoti

Uchumi wa nchi za kipato cha chini umeendelea kupungua:Ripoti

Ripoti ya mwaka 2015 ya kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD kuhusu nchi zinazoendelea LDC imeonyesha kuwa uchumi wa nchi zinazoendelea unadidimia ikilinganishwa na miaka ya awali.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Idhaa hii kufuatia kuzinduliwa kwa ripoti hiyo ya kila mwaka, Mukhisa Kituyi ambaye ni Katibu Mkuu wa UNCTAD amesema ukuaji wa uchumi hivi sasa ni asilimia Tano nukta Tano ikiwa ni pungufu kwa wastani wa takribani asilimia mbili ikilinganishwa na kipindi cha kuanzia mwaka 2002 hadi 2014.

Amesema ripoti imeangazia mataifa matatu ikiwemo Ethiopia, Lesotho na Senegal ili kupata taswira za nchi hizi tatu tofauti kufahamu ni mikakati ipi iwekwe  ili kupunguza umaskini ambapo Bwana Kituyi ametolea mfano wa Ethiopia  akisema ...

(Sauti ya Kituyi)