Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN na wakazi wa Chamwino na mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi:

UN na wakazi wa Chamwino na mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi:

Harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, huko Tanzania zinaendelea ambapo hatua za hivi punde zimegusa mkoa wa Dodoma kwenye kijiji cha Chamwino, ikihusisha mradi wa nishati ya jua.

Mradi huo uliotokana na nguvu za wananchi na fedha kutoka shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP umewezesha wakazi wa kijiiji cha Machali A kupata mradi wa maji kupitia nishati ya jua, sambamba na maji kwa shughuli za kilimo na mifugo.

Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez anafafanua kuhusu manufaa mradi huo alipozungumza na idhaa hii kwa njia ya simu kutoka Dar es salaam.

(Sauti ya Alvaro)