Uthabiti wa ASEAN ni jibu la kukabili changamoto:Ban

Uthabiti wa ASEAN ni jibu la kukabili changamoto:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema uthabiti wa kiuchumi wan chi za Kusini Mashariki mwa Asia, Asean na ushiriki wao kwenye masuala ya kimataifa unaongezeka.

Amesema hayo mjiin Kuala Lumpur, Malaysia wakati wa kikao cha viongozi wa nchi ambapo ameeleza kuwa uthabiti huo utumike katika kukabili changamoto zinazokabili dunia hivi sasa.

Ametaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, uongozi bora, nyuklia na hata vitisho vya usalama vitokanavyo na hali ya usalama mashariki ya Kati, Syria na janga la wakimbizi.

Ban amesema vitisho na changamoto hizo vinaweza kukabiliwa kupitia fursa za kipeke za zama za sasa ambazo ni mazungumzo, kusaidia changamoto na kuzingatia misingi iliyomo ndani ya katiba ya Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu ametaka ushirikiano ili kudhibiti pia migawanyiko na hatimaye kufikia dira mpya iliyomo kwenye ajenda 2030 ya maendeleo endelevu inayotaka utu kwa wote.