Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upatikanaji wa huduma ya choo nchini Tanzania

Upatikanaji wa huduma ya choo nchini Tanzania

Tarehe 19 Novemba kila mwaka, nchi duniani huadhimisha siku ya choo. Hii ni siku inayoangazia umuhimu wa huduma za kujisafi hususani matumizi ya choo kutokana na unyeti wake katika usafi wa binadamu na mazingira yake.

Katika ujumbe wake kwa siku hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema huduma za kujisafi ni kiini kwa usafi wa mwanadamu na mazingira, maendeleo pamoja na utu.

Bwana Ban amesema licha ya hivyo, takwimu hazitii moyo kwani mtu mmoja kati ya watu watatu kote duniani hapati huduma hiyo na mmoja kati ya wanane hujisaidia hadharani. Hata hivyo amesema ajenda ya maendeleo ya 2030 inapigia chepuo huduma za kujisafi na hivyo kutaka jamii ielimishwe na kulindwa dhidi ya hatari ya ukosefu wa huduma za kujisafi ikiwemo magonjwa kama kuhara.

Jijini New York, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika uzinduzi wa ripoti ya maji na huduma za kujisafi iliyo chini ya bodi ya Katibu Mkuu kuhusu suala hilo. Miongoni mwa wajumbe wa bodi ni

Waziri wa Utalii wa Uganda Maria Mutagamba ambaye pia awewahi kuwa waziri wa Maji nchini humo na yeye anasema huduma za kujisafi hususani vyoo zinapaswa kwenda mbele zaidi.