Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wapazia sauti tabianchi katika shindano la muziki

Vijana wapazia sauti tabianchi katika shindano la muziki

Vijana na watoto kutoka Marekani na Indonesia wanajiandaa kwenda Paris, nchini Ufaransa, kuhudhuria kongamano la kimataifa kuhusu tabianchi kati ya Novemba 30 na Disemba 11 mwaka huu, baada ya kushinda shindano la vijana la muziki kuhusu changamoto za dunia.

Shindano hilo la video kwenye mtandao wa intaneti, liliandaliwa na asasi ya kiraia ya Muungano wa Kimataifa wa Kuendeleza Mbinu Bunifu (IAAI), kwa kushirikiana na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Sekritariati ya Mkakati wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, UNFCC na wadau wengine, na washindi walipatikana Novemba 6, 2015, kupitia kura kwenye mtandao wa intaneti na uamuzi wa majaji kutoka mashirika husika.

Vijana hao watapokea tuzo zao kwenye sherehe maalum jijini Paris, mnamo Disemba 7, 2015, kwenye jukwaa la UNESCO.

Katika Makala hii, Joshua Mmali anatumegea kidogo vipande kutoka kwa muziki wa washindi hao.