Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio nchini Mali

Ban alaani shambulio nchini Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la kuogofya katika hotel iitwayo Radisson mjini Bamako Mali, lililouwa watu kadhaa na kujeruhi wengine.

Msemaji wa Katibu Mkuu, Stéphane Dujarric amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa Ban ametuma saalamu zake za rambirambi kwa serikali ya Mali, familia athiriwa na kuwatakia  majeruhi uponyaji wa haraka.

Msemaji huyo amesema Ban amehuzunika zaidi kwani.

(SAUTI DUJARRIC)

‘Ameelezea kusikitishwa kwamba mashambulio yametokea wakati ambapo mchakato wa amani unapiga hatu nzuri na vikundi husika katika makualiano ya amani na mshikamano vilikuwa Bamako kuhudhuria mkutano wa sita wa kamati ya ufuatiliaji wa makataba na na serikali ya Mali na wadau wa kimataifa.’’

Amesema Bwana Ban amelaani jaribio lolote la kufuta utekelezaji wa mkataba  na kuelezea mshikamano waUmoja wa Mataifa kwa Mali katika kupamabana na ugaidi na vikundi vyenye misimamo mikali.