Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya kutokomezwa, Ebola yaripotiwa tena Liberia:WHO

Baada ya kutokomezwa, Ebola yaripotiwa tena Liberia:WHO

Visa vipya vitatu vya Ebola vimethibitishwa nchini Liberia ikiwa ni zaidi ya miezi miwili na nusu tangu nchi hiyo itangazwe kutokomeza ugonjwa huo uliotikisa Afrika ya Magharibi tangu mwezi Machi mwaka jana.

Mwakilishi maalum wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO kwa ajili ya Ebola, Bruce Aylward, ametangaza hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi akisema ni watoto watatu wa familia moja, wakazi wa kitongoji cha Paynnesville, Mashariki mwa mji mkuu wa Liberia, Monrovia.

Amesema kwa sasa familia ya watoto huyo inachunguzwa na kwamba WHO..

(Bruce-1)

‘Tumeongeza muda wa ufuatiliaji wa kina wa Ebola kwa siku 90 zaidi kujaribu kuhakikisha hakuna aina mpya ya njia ya maambukizi inayoweza kuibua dharura mpya.”

Bwana Aylward amesema serikali nayo imeshachukua hatua tangu jana kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.

(Sauti ya Aylward)

“Tayari wamehamasisha vikundi vinavyofuatilia na kubaini iwapo kuwa watu walikuwa na magusano na mtoto huyo, na yote yalifanyika jana saa chache baada ya taarifa za kuwepo kwa mgonjwa huyo.”