Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi hubeba mizigo wasiyostahili: Eliasson

Wakimbizi hubeba mizigo wasiyostahili: Eliasson

Madhila wanayokumbana nayo wakimbizi katika dunia yenye migogoro ni mzigo wasiostahili kuubeba amesema Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson.

Akiongea katika mkutano kuhusu njia za kuboresha namna za kushughulikia janga la wakimbizi , Bwana Ealisson amesema mashambulizi ya kigaidi katika siku za hivi karibuni sehemu mbalimbali yakumbushe ulimwengu kuwapokea salama wakimbizi kwa kuzingatia sheria za kibinadamu na za wakimbizi.

Kuhusu usalama wa wakimbizi anasisitiza.

(SAUTI ELIASSON)

‘Wanaokimbia migogoro hii wasiadhibiwe mara mbili. Kwanza kwa vita au nguvu kandamizi inayowatesa nyumbani, pili kwa unyanyapaa hatari ambao pia huwahusisha wakimbizi na washambuliaji.’’

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa wakimbizi anayemaliza muda wake , Antonio Guterres amesema suluhula kweli la kupepuka wakimbizi ni kuzuia migogoro na pia kusaka suluhu la kisiasa katika maeneo ambapo migogoro inafukuta.

Amesema dunia lazima ifahamu kwamba hakuna mshindi katika vita kwani pande zote zinapoteza.